OFA BAAAAAB KUBWA

Sunday, June 7, 2015

AFYA YETU LEO: JINSI YA KUBORESHA MUONENO WA USO WAKO,KUONDOA CHUNUSI NA MABAKA KATIKA NGOZI YAKO BILA KUTUMIA KEMIKALI




        JINSI YA KUTENGENEZ USO UKIWA NYUMBANI

1. Chukua maziwa ya mgando na utumie kusafisha uso wako.
2. Scrub kwa kutumia mchanganyiko wa mlozi na karoti au mlozi wa jani la chai.
3. fanya toning na maji vuguvugu yaliyochanganywa na kipande cha limao na weak kidogo katika taulo la pamba na futa uso wako mahali pote kasoro penye tatizo.
4. Tumia ute mweupe ambao utakuwa umemwagia katika taulo lako na kujisugua taratibu.
5. Jisafishe na maji ya vuguvugu
6. Fanya toning tena kama ilivyokuwa katika hatua ya tatu juu
7. Ili kuondoa ukavu wa ngozi, kata matango na yabandike katika ngozi.


   NAMNA YA KUONDOA VIPELE NA MAFUTA USONI

         Ukiwa mwanaume au mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili kukuweka mtanashati na mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
           Scrub ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii huondoa upele, chunusi na mabaka usoni.


                                        UONDOAJI WA CHUNUSI KWA NJIA YA ASILI


         Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwena madoa kwa kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kusaidia.
Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainikachanganya na asali, paka usoni.
Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilikakwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamojana krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju.
Sabuni hiyo iko katika boksi kubwa na kwa ndani inakigunia ambacho kinasaidia kusaficha uso, usinunue sabuni ya ukwaju na asali ambayo haijafungwa kwenye kitambaa kigumu chenye rangi ya kahawia itakuwa ni feki na haitakusaidia.
         Kama unataka kupunguza tumbo au mwili kwa ujumla.Asubuhi kunywa chai nzito, mchana kula chakula kilichokamilika.
Ila usiku kula matunda tu ili uweze kuupa mwili nafasi ya kujitengeneza na hasa kupunguza mfuta yaliyozidi mwilini.
Uwe unakula wakati unasikia njaa tu unapokula bila yakusikia njaa unakuwa unarundika tu chakula mwilini na baadaye chakula hicho hubadilika na kuwa mafuta ambayo
hutengeneza manyama uzembe.
Ukishindwa hivyo nenda kwa daktari iliakupe masharti ya vyakula na uweze kupunguza mwili


    JINSI YA KUTUMIA LIMAO KUONDOA CHUNUSI USONI

           KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa ijitengeneze yenyewe na si kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani. Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi nzuri jambo ambalo ni gumu.Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa makavu jambo ambalo linaashiria kuwa kupaka cream  si suruhisho la kuwa na ngozi nzuri.

            Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na kutumia make up kwa muda mrefu  na hata anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni  pia mashavuni kwa kujitibu na juisi ya limao.

Namna ya kufanya
           Chukua  limao lioshe na kisha likamue na kuchuja mbegu zake. Weka juisi hiyo kwenye kikombe na kisha tafuta kitambaa laini  kichovye kwenye juisi ya limao na dondoshea juisi ya limao kwenye sehemu zenye tatizo.
Kaa  kama dakika tano kisha usha uso kwa maji safi.Pia unaweza kuchanganya na asali mbichi  na maji ya limao husaidia pia kuondoa madoa usoni.
Limao lina sifa kubwa ya kuzuia harufu pia unaweza kulitumia katika kuondoa harufu kali ya jasho mwilini  na husaidia kuondoa weusi kwenye kwapa, chini ya macho, mapajani pia.
Chukua kipande cha limao  weka sukari kidogo, sugua.Unatakiwa kutumia kwenye kwapa ambalo ni safi, vizuri kutumia njia hii kabla na baada ya kuoga.



KWA HUDUMA ZA SALOON KAMA VILE MAKEUP NA UPAMBAJI WA MAARUSI,UPAMBAJI WA KUMBI ZA SHUGHULI MBALIMBALI NA UANDAAJI WA KEKI PAMOJA NA KADI ZA HARUSI, WASILIANA NASI ROYAL FASHION DESIGN KWA NAMBA 0654700661


No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!