OFA BAAAAAB KUBWA

Wednesday, July 15, 2015

MADA YETU LEO: UJASIRIAMALI| MBINU SITA ZA UJASIRIAMALI | JIFUNZE MBINU ZA KUKUZA NA KUIMARISHA BIASHARA YAKO







Watu wengi watajiuliza,ujasiriamali unakuja vipi katika site ya mitindo? Unatakiwa ufahamu kuwa Fashion ina mawanda mapana sana..fashion ni maisha kwa ujumla,sio tu mavazi na muonekano wa nje ,bali inahusiana pia na shughuli za kijamii na changamoto zinazoikumba jamii kwa ujumla wake...ndio maana designers,models na mamiss hushiriki kazi mbalimbali za kijamiii na kutoa misaada mbalimbali kwa watu wasiojieweza na kutoa elimu na mafunzo sambamba na kuleta changamoto mbalimbali za kimaendeleo katika jamii ikiwemo kutoa fursa za ajira binafsi kwa vijana ....sasa tuelekee moja kwa moja katika mada yetu....

Ni mbinu gani au ujuzi wa namna gani ambao mjasiriamali anapaswa kuwa nao?
Zipo mbinu nyingi ambazo mjasiriamali anazipata kadri anavyotumika katika shughuli za kijasiriamali, lakini zipo mbinu chache ambazo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nazo kabla hajafungua "milango" ya biashara. Soma mbinu hizo hapa na ikiwa kama utaona mbinu ambayo unahitaji kuifanyia kazi basi hakikisha unashughulika nayo wakati unaandaa utaratibu wa bishara yako (Business Plan).  Sehemu nyingine itanipasa kuelezea kiingereza kwa kuwa ni ngumu kupata tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili.


1. Kujituma (Self Motivation)
Kitu cha kwanza kabisa ambacho mjasiriamali anapaswa kuwa nacho ni uwezo wa kuamka mapema asubuhi na kufanya kazi zake, kama umekuwa na kawaida ya kuchelewa kazini au masomoni kwa muda wa dakika 10 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, ni dhahiri kwamba itakuwia vigumu kuweza kubadilika kama utaanzisha biashara yako mwenyewe, hapa suala sio kuamka mapema tu, suala ni kuamka mapema, kuanza kazi kwa muda unaopaswa na kumaliza kazi kwa muda huo huo. Panga ratiba yako ya siku nzima, na uifuate ratiba hiyo ipasavyo.

                                                                2. Kujiamini (Self Confidence)
Kila mjasiriamali anapaswa kuwa na imani juu yake mwenyewe, bidhaa zake na biashara yake kwa ujumla, yakupasa kuwa na ufahamu kuwa ni kweli bidhaa zako zinawasaidia watu na kwamba kiasi cha fedha unachowatoza ni kizuri (fair) kwako wewe na kwa wateja wako.

                                                          3. Maadili (Morals and Ethics)
Maadili ni msingi wa kila mjasiriamali mzuri, mwanzoni kabisa mwa biashara yako unatakiwa ufahamu wewe na biashara yako mtasimamia nini na wapi itakuwa ni mipaka yako, wajasiriamali wengi wanashindwa kuendesha biashara zao kwa sababu ya tamaa ya fedha, kama utashindwa kusimamia maadili utajikuta wewe pamoja na biashara yako mkibatizwa majina mabaya kama "Mafisadi" n.k, hakuna mteja au mtu yoyote ambaye angependa kufanya bishara na mtu asiye na maadili mema.

                                                 4. Kutunza Muda (Time management)
Kama nilivyosema kwenye kipendele cha kujituma, unapaswa kupanga ratiba yako na kuhakikisha unaifuata, Wajasiriamali hususani wapya, wanapaswa kufahamu kwamba kila dakika uliyonayo ni ya thamani kwako, wakati wa kuanza biashara utajikuta huna majukumu mengi ya kuweza kukufanya utumie masaa 8 kwa siku, lakini jambo hili halimaanishi utumie masaa 3 kupata chakula cha mchana ukiwa na marafiki zako, tumia muda huu ambao unaona ni wa ziada kutafuta mbinu za kutanua biashara yako, tafuta namna za kutangaza biashara yako na kufanya mawasiliano na wateja wenye manufaa zaidi kwa biashara yako.

                                                                       5. Mauzo (Sales)
Kila biashara ni lazima ifanye kazi kwa mauzo, kila biashara ina namna ya kipekee ya kuweza kufanya mauzo ya bidhaa zake, wewe kama mjasiriamali ni jukumu lako kutazama ni aina gani ya mauzo ambayo unaipendelea kwa ajili ya biashara yako, kama ushawahi kufanya biashara ya rejareja, utakuwa na ujuzi wa wafanya biashara wengi wenye matumaini. Kufaidika vyema na hili, wajasiriamali watapata ujuzi kwa kupitia semina za mauzo, vitabu na programu mbalimbali za kutiana moyo (motivational programs).


6. Fedha (Finance)
Wakati unapokuwa katika biashara, ujuzi wa fedha hauepukiki. Kufahamu jinsi ya kuwizanisha (kubalance)  "checkbook" na kuweka orodha ya ankara zilizokwisha kuhesabiwa (numbered invoices), ni jambo ambalo mjasiriamali mdogo anapaswa kuanza nalo, kitu muhimu kuliko vyote kwa wajasiliamali wadogo ni kupangilia muda, hususan kwa ajili ya kusimamia fedha, na kuutumia vyema huo muda. inafaa sana kuwa na uwezo mzuri wa kutumia software ya usimamizi wa fedha iitwayo QuickBook , japo ujuzi huu sio lazima uwe nao.

Kuzifanyia kazi mbinu hizi kabla hujaingia katika biashara kutakuhakikishia matokeo mazuri ya biashara yako. Kufikia hapo kama una mawazo mazuri ya  biashara, hakuna kitakacho kuzuia kuwa na mafanikio.

Katika kuandaa "Business Plan", ni vyema ukajifunza kutumia software mbali mbali na moja kati ya nilizopitia,  na ambayo nimeona inafaa sana ni software ya palo alto

Natumaini makala hii itawasaidia kwa kiasi fulani Watanzania wenzangu.




                          ROYAL FASHION TANZANIA


           TUNADESIGN NA KUTENGENEZA NGUO KAMA VILE MAGAUNI ,SUTI,YA MITINDO MBALIMBALI,VIATU VYA KITENGE,MIKOBA NA VITU KIBAO…TUNABUNI NGUO MAALUM ZA SHEREHE NA SHUGHULI MBALIMBALI KAMA VILE HARUSI,SEND OFF,KITCHEN PARTY,BIRTHDAY PARTY NA NYINGINEZO.
 BEI ZETU NI POA SANA,KARIBU UPENDEZE..TUPIGIE AU TUCHEKI WHATSAP KWA NAMBA 0654700661

 TU-FOLLOW INSTAGRAM ..BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!