OFA BAAAAAB KUBWA

Sunday, July 5, 2015

UREMBO NA USAFI: Jifunze Jinsi ya kukabiliana na makwapa myeusi (dark underarms) kwa njia rahisi ukiwa Nyumbani.


 ROYAL FASHION TANZANIA


TUNATOA HUDUMA ZA SALOON,TUNAFANYA MAKEUP ZA KISASA ZAIDI, PIA TUNAPAMBA MAHARUSI,TUNAPAMBA KUMBI MBALIMBALI KWA AJILI YA SHEREHE NA SHUGHULI NYINGINE MBALIMBALI.

PIA TUNAUZA MAKEUP FULL PACKAGE,WIVING,RASTA,MAVAZI NA ACCESSORIES MBALIMBALI .NJOO SASA TUKUHUDUMIE MTEJA WETU...WASILIANA NASI KWA NAMBA 0654700661





Mara nyingi makwapa kuwa myeusi husababishwa na kunyoa kwa kutumia wembe au shaving machine mara kwa mara. Ili kuepuka weusi wa makwapa ni vyema kufanya waxing kwa maana hutoa nywele zote kuanzia kwenye mizizi. At times aina ya deodorants na perfurmes tunazotumia pia husababisha makwapa kuwa myeusi kutonaka na aina ya chemicals zinazotumika kuzitengeneza. Kwa mantiki hiyo basi inabidi kuangalia na aina ya hizo deodorant na perfumes unazotumia, na hata ukitumia epuka kuspray perfumes kwenye ngozi kama wewe una tatizo hilo.
pamoja na hayo yote tunaweza kuondoka weusi wa makwapa kwa kutumia vitu asili ambavyo vinapatikana majumbani mwetu.
Nitajaribu kukuorodheshea baadhi ya tiba za nyumbani kwa ajili ya kuondoa weusi makwapani:
  • Chukua kipande cha limao na usugue kwenye makwapa yako. Osha baada ya dakika 15. Limao ni bleach asili inayosaidia kusafisha ngozi nyeusi.
  • Baada ya kuoga vizuri chukua baking soda na upake kwenye makwapa yako, nayo pia inasaidia kutoa weusi kwenye ngozi.
  • Unaweza pia kutumia aloe vera gel au mafuta yenye Vitamin E ni tiba asili ya kusafisha ngozi nyeusi.
  • Sugulia mchanganyiko wa liwa na maji ya rose, kaa nayo mpaka ikauke kisha osha.Liwa ni tiba nzuri sana ya ngozi na pia huifanya ngozi kuwa nyororo.
  • Chukua kijiko kimoja cha chai cha maji ya tango na kijiko kkimoja cha chai cha maji ya ndimu, changanya na manjano kidogo upate mchanganyiko mzito kidogo, paka,kaa nayo kwa muda wa dakika 20 kisha ioshe.

Njia ya Asili ya Kulainisha Ngozi

Wanawake wengi wanapenda kufanya miili yao kuwa na ngozi nyororo, lakini tatizo linaku kwenye vipodozi wanavyotumia.
Unaweza kuepuka matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa ngozi na mwili wako kwa kutumia njia rahisi na za asili katika kulainisha ngozi yako.
Kujipodoa kwa njia za asili ni vizuri zaidi, kwa vile hakuna kemikali zozote zitakazokusababishia matatizo katoka ngozi na mwili wako. 
Tuangalie jinsi ya kulainisha ngozi kwa kutumia tui la nazi pamoja na asali.
Jinsi ya kufanya:
  • Kuna kipande kimoja cha nazi, kisha weka maji kidogo na kuchukua ili upate tui zito.
  • Weka tui hilo zito kwenye chombo kisafi na uchukue asali yako kisha changanya na lile tui
  • Changanya huo mchanganyiko mpaka uwe mzito
  • Baada ya hapo paka mchanganyiko huo kwenye ngozi yako huku ukisugua taratibu. Hakikisha hutumii nguvu nyingi
  • Kaa nayo kwa muda wa saa moja baada ya kusugua mwili wako kwa kutumia mchanganyiko huo, kisha unaweza kwenda kuoga na kuendelea kupaka mafuta ya aina yoyote ya ngozi unayopendelea kutumia.
  • Ukiendelea na zoezi hili kwa muda mrefu ngozi yako itakuwa laini na nyororo








 ROYAL FASHION TANZANIA


TUNATOA HUDUMA ZA SALOON,TUNAFANYA MAKEUP ZA KISASA ZAIDI, PIA TUNAPAMBA MAHARUSI,TUNAPAMBA KUMBI MBALIMBALI KWA AJILI YA SHEREHE NA SHUGHULI NYINGINE MBALIMBALI.

PIA TUNAUZA MAKEUP FULL PACKAGE,WIVING,RASTA,MAVAZI NA ACCESSORIES MBALIMBALI .NJOO SASA TUKUHUDUMIE MTEJA WETU...WASILIANA NASI KWA NAMBA 0654700661




No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!