Majaji kwa Upande wa wabunifu wa Mitindo-Mavazi na Upigaji wa Picha wakiwa wanaendelea na kazi za uhakiki wa Majina ya kuwapata washiriki 20 ambao wataingia katika Shindano hilo.
Mbunifu na Mwanamitindo wa Mavazi ambaye pia ni Balozi wa Fasdo Martin kadinda akiongea kwa niaba ya Majaji upande Majaji wa Mitindo akielezea jinsi mchakato ulivyo kwenda.
Jaji katika upande wa kupiga Picha Sameer Kermalli akizungumzia mchakato mzima walioufanya kuwapata washiriki ambao wataingia katika shindano kwa upande wa upigaji picha
Majaji upande wa kupiga picha wakiendelea na Mchakato wa kuwapata washiriki 10 ambao wataingia katika ushiriki wa kumpata mshindi wa upande wa kupiga picha.
Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa akizungumzia mchakato mzima wa shindano la Bongo style Competition
Kuelekea Shindano la Bongo Style Competition , Ambalo linatarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwezi wa Kumi na moja mwaka huu, Majaji wamefanikiwa kuwapata washiriki ambao wataingia katika Kinyang'anyiro hicho
Katika Mchakato huo Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande ambaye ndiye alikuwa ni msimamizi mkuu wa mchakato huo alisema kuwa mchakato ulienda sawa, na kwa pande zote walitumia vigezo stahiki kuwapata washiriki 20 ambao wanaingia katika shindano hilo, Pia aliwashukuru Culture and Development East Africa(CDEA) kwa kutoa ukumbi kwa ajili ya kufanyia kazi pamoja na wapiga picha.
Akizungumzia Shindano hilo Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema shindano hilo linalengo la kuibua vipaji vya vijana wenye kati ya umri wa miaka 18-25 katika nyanja za ubunifu mitindo na upigaji picha ili kuwahamasisha kutumia vipaji vyao kujiajili wenyewe. Aliongeza kuwa idadi ya Fomu zilizotumwa kwa njia ya mtandao zilikuwa 310 kati ya hizo zilizo pitiwa na Majaji pande zote ili kupata washiriki 20 zilikuwa fomu 285.
Nae Jaji wa Eneo la Mitindo Ambaye pia ni Balozi wa FASDO Martin Kadinda alizungumzia shindano hilo kuwa ni zuri na lipo kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya wanamitindo na kuongeza pia wale wote walioshiriki katika Shindano hili hasa walioleta fomu zao walikuwa wanauwezo lakini kwa kuwa ni shindano wachache ndio walikuwa wanatakiwa kulingana na vigezo na Masharti walivyoweka.
Akiongezea Jaji upande wa Picha Sameer Kermalli kwa niaba ya majaji wengine amesema kuwa wamepokea na kupitia picha za washiriki wengi walioleta picha wamepitia na kugundua baadhi yao wamepiga picha nzuri ambazo zipo kitaalam na wengine wamepiga picha ka kuzi nakshi sana jambo ambalo limesababisha kupunguza alama zao na pia wengine wametumia picha ambazo sio zao, aliongeza kwa kusema baadhi yao ambao wamechukuliwa wamefanya vizuri kutokana na ubunifu wao.
Philipo Florian ambao wapo katika mitandao ya kijamii na waliokuwa wakipokea fomu hizo, alisema kuwa fomu nyingi zilikuja kwa kurudiwa rudiwa kitu ambacho kilichanganya kidogo mchanganuo, pia watu wengi walipaa shida wakati wa kuweka Picha lakini hata hivyo wengi walifanikiwa na kushiriki kikamilifu. Pia Anna Semiono aliongeza kuwa zoezi lilienda kikamilifu na idadi ya wanawake na wanaume ambao walileta fomu zilikuwa sahihi ingawa baadhi yao walikosea kwa namna moja au nyengine kutokana na kuto elewa vizuri ni namna gani wangeweza wasilisha kazi zao, hata hivyo alisema changamoto hiyo haitakuwepo katika shindano lijalo kwa kuwa kutakuwa kuna elimu mbadala kupitia VIDEO CLIP itakayo onesha namna ya kutuma kazi zao.
ROYAL FASHION TANZANIA INAWATAKIA KILA LA HERI WASHIRIKI WOTE KATIKA HATUA ZINAZOFUATA
No comments:
Post a Comment