OFA BAAAAAB KUBWA

Wednesday, December 2, 2015

BARRISH FASHION DARASA : FAHAMU VITU MUHIMU KABLA YA KUFANYA MAKE UP


MAKE UP



Make up mara nyingi imekuwa ikitumika kama sehemu ya UREMBO kwa wanawake na wanaume wanaopenda kwenda na wakati kwa ajili ya kufanya muonekano wa ngozi yao kuwa bora na yenye kuvutia.Kuna make up za aina mbili. Make up aina ya Kwanza  ni kisasa inayotumia vipodozi na rangi, na ya pili ni ile ya kiasili ambayo hutumia Matunda ya aina mbalimbali,mafuta ya nafaka za aina mbalimbali pamoja na cream ya maziwa ya wanyama mbalimbali.
jjjl
Hadi hivi sasa kumekuwa na aina nyingi za makee up kwa matumizi mbali mbali ,ikiwa ni kwa ajili ya urembo,kupata muonekano wa tofauti mfano katika filam,show za muziki,show za mitindo n.k .Lakini Leo hii sisi katika mada yetu ya leo  tutajikita katika kuangazia make up kwa ajili ya UREMBO wa kawaida kwa watu wote.Mara nyingi mtu anapofanya make up usoni ,utofauti hujitokeza kutokana na aina ya kipodozi hicho kufanya kazi ya kung’arsha na kupendezesha ngozi ya uso.

UNAPO HITAJI KUFANYA MAKE UP NI LAZIMA KUZINGATIA MAMBO YAFUATAYO :

-Aina ya make up
-Ubora wa vipodozi kulingana na mahitaji ya muonekano wako kwa muda huo .
-Vipodozi na rangi zinazoendana na rangi ya ngozi yako
IZINGATIWE kuwa watu wenye ngozi za mafuta mara nyingi wamekuwa wakishauriwa kutumia make up za poda au zilizo katika mfumo wa unga unga pamoja na vipodozi vilivyotengenezwa kwa viambatanishi vya cytrus [machungwa na limao] ili kuweza kukausha mafuta ndani na juu ya ngozi yako.
Hii husaidia kufanya ngozi yako kuwa kavu kwa muda mrefu na kufanya ngozi kupumua vizuri kwa matundu yake kuwa wazi bila kubugudhiwa na mafuta ya ngozi au uchafu mwingine .Ni tofauti na kama mtu huyo mwenye ngozi yenye mafuta mengi akitumia Make up ya cream ,kwa aina hii ya make up inaweza kuziba vitundu vya hewa katika ngozi ya uso na kupelekea kusababisha ngozi ya uso kupata vipele /chunusi
Kwa kumalizia ningependa pia kutoa angalizo au ushauri kwa watu wenye ngozi kavu.Mara nyingi watu wenye ngozi kavu wamekuwa wakiishi kwa kujisahau katika kutumia aina za mafuta na vipodozi ,kwa kuwa mara nyingi wao ngozi zao huwa si rahisi kuharibiwa na vipele au hali yoyote ile..Katika hilo ,ni vizuri nao katika make up wapendelee kutumia make up ya poda ,na si ya cream au mafuta mara kwa mara .Kwani hata hivyo make up ya cream katika ngozi si yenye kukaa kwa muda muda mrefu sana kama zaidi ya masaa ma nne bila kuonyesha hali wa kupotea ila make up kavu /poda inaweza kustahimili usoni kwa zaidi ya masaa hayo na uso ukawa safi.
Hakikisha unapaka make up huku uso wako ukiwa safi,ili kuifanya ngozi yako kuwa tayari na kustahimili aina ya UREMBO unaowekwa ndani yake.Kumbuka kupaka make up kwa kutumia vifaa vyake kama brash ,kitambaa maalumu n.k. Kwa wale watumiaji wa make up za vipodozi vya madukani vyote hivyo vinapatikana katika seti ya make up,lakini wale wenzangu na mimi wa make up za asili tujitahidi kupata brash safi au kitambaa safi.

IMEANDIKWA NA ; BARISH HOLLIC TZ
MHARIRI : JOSH DESIGNER 0654700661

No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!