OFA BAAAAAB KUBWA

Sunday, December 6, 2015

HIZI NDIZO AINA TANO ZA MAVAZI YA KIAFRIKA YANAYOVUTIA ZAIDI, TAZAMA HAPA


BARISH ONLINE FASHION DARASA















Kwa kawaida kila bara na kila nchi hapa duniani wamekuwa na aina yake ya mavazi asilia kama sehemu ya urembo na mitindo kiujumla .Kwa upande wa UREMBO na mitindo asilia ya mavazi ndani ya nchi za ki Afrika,kumekuwa na namna tofauti tofauti ya vitambaa ,mwonekano,ushonaji na uvaaji.Yote hiyo ikilenga katika kuketa ladha ya kipeee ndani ya mwonekano wa mavazi.
Pengine kunaweza kuwa na aina nyingi ya mavazi asilia katika nchi za bara la africa ,lakini kwa upande wetu leo hii tunajikita zaidi katika kuelezea aina ya mavazi.

Wema Sepetu katika ubora wake

 
:AINA 5  ZA MAVAZI YA KIAFRIKA :

1.KITENGE
2.BAZEE
3.BATIKI
4.KHANGA
5.MAKENZI

KITENGE
Hili ni aina ya vazi ambalo asili yake ni Afrika ,na material yake ni yenye uasili wa kudumu na kuvutia.
         
Vazi la kitenge,kwa miaka kadhaa tangu lianze kutumika limekuwa likijipatia ubora na nafasi ya kipekee katika kukua na kuendelea zaidi.Wanaume kwa wanawake wamekuwa wakishona mavazi ya kuendana nao ya kisasa na yakuwafanya wawe wenye kuvutia .
    
Na nzuri zaidi KITENGE kutokan na mahitaji yake kuzidi kukua,mara nyingi imefikia hadi sasa watu kupenda kulitumia vazi hilo katika sherehe mbali mbali na mionekano tofauti.
Uzuri wa KITENGE ,hupelekea kupatikana kwa aina nyingi ya mishono ndani yake .



Gauni refu maalumu kwa shughuli mbalimbali lililotengenezwa kwa kitenge
Kitenge kinaweza kuchanganywa na nguo nyingine na kuvutia zaidi

Kwa urembo zaidi ni ndani ya muonekano wa kitenge ,kilicho shonwa kwa mitindo ya kipekee na kuvutia

 .
BAZEE
vazi hili pia halina tofauti sana na kitenge katika sifa na ubora wake .Kwani takribani asili ya mavazi yote ya ki Afrika yapo kwa ajili ya kupendezesha na kuboresha mwonekano halisi wa mwafrika

Vitambaa vya bazee vimekuwa vikipatikana kwa namna tofauti tofauti kuanzia ukubwa ,rangi zake na maua yake.Yote hiyo ni kufanya muonekano wa kipekee na kuzidi kung’ara
Mpaka sasa hivi tumekuwa tukishuhudia idadi ya watu wengi wakipendelea kushona na kuvaa vazi hilo la bazee katika sehemu tofauti za mikutano,seherehe,harusi n.k kwani lina mvuto wake asilia kutokana na ulivyoamua kushona

BATIKI
katika vazi hili uzuri wake huanza kuonekana pale baada ya kutengenezwa kwake kwa namna ya uchanganyaji rangi tofauti tofauti ,ambazo mwonekano wake hujitokeza kama nakshi za maua maua .
Vazi hili pia humruhusu mtu yoyote yule kukidhi mahitaji yake ya aina au mtindo wa mshono ambao anauhitaji kwa muda muafaka .


MAKENZI
Aina hii ya nguo,kidogo kwa idadi ya watu wengi tulio zaliwa miaka ya hivi karibuni ,limekuwa geni kwetu japo sio sana.Kwani uvaaji wake kwa idadi ya watu WENGI haukuwa sana ,hadi kupelekea kizazi cha Leo kutoliona pendwa na lenye thamani .

Ila vazi hili tena limekuja kupata umaarufu kwa kujulikana na idadi ya kundi la watu hivi karibuni tena,ambapo wahusika wa kushona (mafundi)/designers kulitumia mala kwa mala na katika aina tofauti tofauti za mitindo ya nguo inayo kwenda na wakati. nguo ya kawaida ikichanganywa na vitambaa hivyo na kuifanya iwe yenye kuvutia .

makenzi

KHANGA 
Vazi hili waswahili wamezoea kuliita jumba la fahari ya maneno .Hii ni kutokana na aina ya upambaji wake unavyo kuwa ,maua yenye rangi tofauti tofauti,ukubwa unao jitosheieza mtu kujifunga au kushona na maneno yake yalivyo ambatana ndani yake.

UZURI WA KHANGA : Khanga inatoa nafasi nyingi kwa matumizi ya watu wote haswa wanawake .Kwa idadi kubwa ya maisha yao yote ya wanawake /mtoto wa kike hutumia vazi la khanga,kujifunga,kubebea mtoto,kushona na kazi zingine .
Pia vile vile kwa upande wa mwanaume /mtoto wa kiume vazi hili linapata nafasi ya kutumika pale anapo pata tohara,kujifunga kwenda kuoga ,pia hata kushona kama shati ,kaptula na suruali.

Khanga kwa gauni lenye nakshi nakshi za urembo ,pia lilo wahi kutumika katika Swahili Fashion Show


Khanga inakupa Uhuru sana kutokana na wepesi wa material yake yaliyoitengenezea ,kuifanya kuwa nyepesi inayo ruhusu kupitisha hewa na kuitumia kwa namna yoyote.
Huo ndio uasiri wa mwafrika katika mavazi ya asili yanayo wakilisha soko la urembo na mitindo duniani kote.Fahari ya mwafrika ni kujivunia katika kilicho bora .
Kwa mavazi ya aina zote hapa katika ukurasa wetu unaweza ukapata kwa simu no: 0654700661

No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!