OFA BAAAAAB KUBWA

Sunday, June 19, 2016

UREMBO NA USAFI: USAFI WA SURA | USO


NGOZI katika urembo, ni eneo muhimu na linalochukua sehemu kubwa ya urembo kwa wanawame kuliko maeneo mengine ya mwili.
Hilo linatokana na ukweli kuwa kama isipotunzwa vizuri, basi muonekano wote wa mtu utakuwa si mzuri, kutokana na hali hiyo basi ni vyema kuhakikisha unaipa ngozi yako umuhimu mkubwa katika matunzo.

Urembo wa ngozi unahusisha sehemu nyingi za mwili, lakini leo tutaangalia uhumimu wa kutunza ngozi ya uso wako, kwani uso ndio kila kitu, wengi wanaita ‘reception’ na kama ngozi ya uso wako haitakuwa na muonekano mzuri, basi hata urembo wako pia utakuwa mashakani.
Matunzo ya uso yanahitaji umakini na ufuatiliaji wa karibu kwani ni eneo linalokabiliwa na changamoto nyingi katika mwili hasa kwa watu wenye ngozi za mafuta.Kwa kuzingatia kuwa uso ndio ukaribisho kwa mtu yeyote linapokuja suala la urembo, ni muhimu kuhakikisha kuwa ngozi yako inakuwa katika hali nzuri na safi wakati wote.


Hakikisha unatenga walau dakika kumi kila siku asubuhi kwa ajili ya usafi wa ngozi ya uso wako.
Unapoamka asubuhi, safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na utumie sabuni uliyoshauriwa na mtaalamu au unayotumia kuoshea uso wako mara kwa mara.
Pia epuka kutumia sabuni ya kipande, kwani hijatengenezwa maalumu kwa ajili ya uso na huweza kufanya ngozi ya uso kukomaa na kupauka.


Ni kawaida ngozi ya uso kuonekana iliyochoka hasa inapofika jioni, baada ya mizunguko ya kutwa nzima, hivyo basi ili kuhakikisha unakuwa na ngozi ya uso iliyochangamka wakati wote kwa kuiosha, lakini unatakiwa kuwa makini zaidi katika hili.


Hakikisha unaosha uso wako vizuri wakati unaoga au wakati unanawa bafuni au popote panapofaa baada ya mizunguko yako ya kutwa.
 Tumia kitambaa au kitu laini kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu ulioganda usoni.Zoezi hili linatakiwa kufanywa kwa uangalifu ili kuhakikisha hauchubui wala kujiumiza ngozi, hakikisha ngozi yako haiwi na magamba ya aina yoyote kwani lengo la kutunza ngozi ni iwe na unyevunyevu na ya  kuvutia.



Unaweza kutumia ‘tona’ kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu ulioganda.
Jambo kubwa la kuzingatia ni kuhakikisha haulali na vipodozi ulivyopaka asubuhi au mchana, kwani husababisha ngozi yako kukosa hewa.
Kwa matokeo mazuri ya afya ya ngozi ya uso wako, zingatia usafi, kunywa maji mengi na kula mboga za majani na matunda kwa wingi.

No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!