Maandalizi ya harusi yamekuwa magumu na yenye kuchosha sana kwa sababu watu wengu hawajui ni wakati gani waanze na kipi kifanyike kwa wakati gani. Matokeo yake waoaji na waolewaji wanakuwa ‘busy’ sana siku za mwisho na kukosa muda wa kupumzika wakielekea kwenye harusi yao. Hapa kuna maelekezo machache ya jinsi ya kupangilia mambo yako ya sherehe ya harusi ili kuepuka kukimbia kimbia dakika za mwisho.
Mwaka mmoja hadi miezi tisa kabla
1. Panga tarehe ya harusi na mahali pa kufanyia
2. Anza kujiandaa kifedha na jinsi gani utapata msaada wa kifenda na kimaandalizi.
3. Panga ni aina gani ya harusi mnayoitaka kulingana na uwezo wenu.
4. Hakikisha umekamilisha mambo yote ya kifamilia na andaa pete ya uchumba kama bado.
5. Waeleze ndugu na marafiki wa karibu mapango wako wa kufunga ndoa na tarehe uliyoichagua.
6. Andaa wasimamizi wa harusi na uwataarifu ili wajipange mapema.
7. Kama mwanaume unaishi na wazazi / ndugu ni muda muafaka wa kutafuta na kuhamia kwako.
Miezi nane hadi sita kabla
1. Tafuta ukumbi na lipia hela ya mwanzo, ‘advance’.
2. Kama ‘engagement’ bado haijafanyika ni wakati muafaka wa kufanya hivyo.
3. Chagua rangi ya harusi, kama nguo ni za kununua au kushona huu ndio muda wa kuanza kuzitafuta na kutafuta mshonaji.
4. Tafuta wapiga picha, wapishi, wapambaji na MC wa shughuli hiyo.
5. Andaa kamati ya maandalizi na kuanza maandalizi ya awali.
6. Panga mahali pa kufanyia fungate na uanze maandalizi pamoja na kuweka akiba kwa ajili yake.
7. Kama utahitaji maids huu ndio wakati wa kuwaandaa.
Miezi mitano hadi mitatu kabla
1. Nunua viatu, accessories na vitu vyote vinavyohitajika kwenye harusi pamoja na vya maids.
2. Andaa listi ya ndugu ambao watahudhuria harusi yako kutoka mbali na mahali inapofanyika na usafiri pamoja na malazi yao.
3. Anza kuandaa vitu vitakavyohitajika kwenye fungate.
4. Anza vikao vya maandalizi.
5. Sambaza kadi za michango kwa wote ambao unawatazamia wakuchangie.
Miezi miwili hadi mmoja kabla
1. Pima nguo za harusi na fanya marekebisho yote yanayohitajika, pamoja na maids.
2. Pitia bajeti na uone kama vitu vyote vinavyohitajika vinawezekana kupatikana.
3. Andaa magari yatakayohitajika kwenye sherehe.
4. Weka oda ya keki ya harusi.
5. Malizia malipo yote ambayo bado hujakamilisha yabaki yale ya kulipia mwishoni tu na tenga fedha zake kabisa.
6. Fanya ‘booking’ ya saluni hasa kwa bibi harusi.
7. Kama hujakamilisha maandalizi ya fungate hakikisha unayakamilisha sasa.
8. Kama mwanaume unaishi na ndugu/ jamaa nyumbani kwako ni muda muafaka wa kuwaondoa ili mkeo akija baada ya harusi akukute peke yako.
9. Nunua pete za harusi
Mwezi wa mwisho
1. Andaa watu wa kushughulikia mambo yote ya ukumbi,chakula, vinywaji, picha, MC, usafiri n.k ili uweze kupumzisha mwili na akili yako.
2. Sambaza kadi za mwaliko
3. Pata muda wa kutosha kupumzika, chukua likizo wiki ya mwisho kuelekea harusi yako.
4. Kama nguo zilikuwa kwa fundi, pima kwa mara ya mwisho na kuzichukua.
5. Vaa viatu vyako vya harusi na utembee navyo ndani ya nyumba kuona kama vipo ‘comfortable’.
6. Onana na MC na mpange utaratibu wa sherehe nzima.
PICHA KWA HISANI YA | http://www.mcluvanda.com
TANGAZO
ROYALA FASHION TANZANIA TUNAFANYA WEDDING PLAN: TUPO KWA AJILI YA KUHAKIKISHA HARUSI YAKO INAKWENDA VIZURI ,INAPENDEZA NA KUWEKA HISTORIA NZURI NA KUBWA KATIKA MAISHA YAKO.SASA USIUMIZE KICHWA,ROYAL FASHION TUNASHUGHULIKIA KUPLAN HARUSI YAKO KUANZIA HATUA YA MWANZO MPAKA MWISHO KWA KILA HUDUMA UNAYOSTAHILI KUIPATA KAMA VILE MAANDALIZI YA UKUMBI, MAVAZI, MC ATAKAEHOST SHUGHULI YAKO, WASIMAMIZI WAZURI, UPAMBAJI , MAKEUP ZA MAHARUSI , USAFIRI ,STILL PICTURE NA VIDEO SHOOTING NA KADHALIKA.
UNAWEZA KUWASILIANA NASI SASA KWA NAMBA 0654700661 AU EMAIL: royalfashion@gmail.com
No comments:
Post a Comment