OFA BAAAAAB KUBWA

Thursday, July 28, 2016

UNATAMBUA KILICHOPO KWENYE MEN’S FASHION TREND?


MEN’S FASHION TREND
Siku zote linapokuja swala la kuzungumzia au kuangalia ni aina gani ya mavazi kwa wanaume yanakuwa yapo ndani ya wakati kwa muda huo (fashionable). Basi tunajaribu kuyaangalia katika sehemu tatu tofauti :Vazi maalumu (Formal Wear), Vazi la kawaida (Casual Wear) na Vazi la ufukweni (Beach Wear).
VAZI MAALUMU (Formal Wear) .
Aina ya vazi hili huvaliwa sehemu tofauti kutokana na tukio na matukio hayo yanajulikana kama Formal Social Events. Vazi hili huvaliwa kutokana na sehemu unayokwenda na kuzitaja chache ni kama Wedding, Formal Garden Party, Dinner etc. Vile vile matukio hayo hutumika sana na Nchi ambazo hazina Vavi la Taifa au kutokana na hali ya hewa.
 IMG_20160626_015555
IMG_20160626_010158IMG_20160626_015555
Ndani ya muonekano wa mavazi haya kama mwanaume unakuwa katika hali ya kuvutia, kupendeza na kuonekana mtanashati zaidi.
VAZI LA KAWAIDA (Casual Wear).
Hapa ni aina yote ya mavazi ambayo yanakufanya muda mwingi unakuwa huru kutokana na aina yake, jinsi ilivyo tengenezwa au wewe mwenyewe kupenda. Pensi (short), Kauwoshi (Sleeveless), Crazy jeans (Ripped Jeans), Pull over, Kofia (Hat) n.k
Na pia aina hii ya vazi ndio pekee au mara nyingi hukupa nafasi ya kuendea Club au sehemu nyingine za starehe na bado ukaonekana unapendeza na kuvutia kwa mazingira husika.
IMG_20160626_014903IMG_20160626_014959 IMG_20160626_014959
Pia ieleweke kwamba mitindo ya muonekano wa nguo za wanaume huwa haibadiliki sana kama tunavyo weza kuona kwa wanawake. Bali tu kinacho chukua nafasi kwa mitindo ya nguo za kiume ni uboreshaji na kuongezea baadhi ya vitu vidogo vidogo tu.
Ukichukulia mavazi kama jeans yamekuwepo kwa muda mrefu sana hubadilika majina na style, T-shirt na jeans imekuwepo tokea miaka ya 1960 mpaka leo. Viatu kama Timberland, Nike Airforce One, Converse AllStars au Air Jordans ni vitu ambavyo vimekuwepo na vikivaliwa kwa miaka mingi sana tokea miaka ya 1980 na imerudi kuwa famous tena.
IMG_20160626_014634
VAZI LA UFUKWENI (Beach Wear).
Kwa wanaume wanapokuwa ufukweni au sehemu zingine za kuogelea, basi aina ya mavazi haya ndio kwa kiasi kikubwa yanachukua nafasi. ambapo ukiangalia hubadilika rangi na kuongezewa vitu vidogo vidogo kama nilivyosema hapo mwanzoni.
IMG_20160626_014526 IMG_20160626_014634
Karibu kwa maoni na ushauri, au kama unahitaji kushauriwa kuhusiana Men’s Fashion wasiliana nami kwenye info@gongamx.com.
ASANTE SANA
Barrish Hollic
FASHION WRITER

No comments:

Post a Comment

HARUSI | WEDDING OUTFITS

TUNASHONA NA KUDARIZI

Royal Fashion Tanzania

ZILIZOBAMBA ZAIDI

Lady in Red | Gauni nzuri,What a beautiful dress

 Karibu upendeze, Wasiliana nasi 0654700661 (Whatsapp)

ASANTE SANA KWA KUTUTEMBELEA. KARIBU TENA!